WATUHUMIWA MAUAJI WATOTO WA TATU KIJIJI CHA IKANDO WAFIKISHWA MAHAKAMANI

   
- HD качество

WATUHUMIWA MAUAJI YA WATOTO WATATU KIJIJI CHA IKANDO WAPANDISHWA MAHAKAMANI Watuhumiwa watatu wa mauaji ya watoto watatu katika kijiji cha Ikando wilayani Njombe wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Njombe ambapo kesi hiyo imetajwa kwa mara ya kwanza . Majira ya saa tano asubuhi watuhumiwa wamefikishwa mahakamani wakitokea katika kituo cha polisi cha mji wa Makambako ambapo Hali ya Ulinzi ikiwa imeimarishwa Mahakamaniu hapo. Wakili mwandamizi wa serikali mkoa wa Njombe Ahmed Seif ameiambia mahakama kuwa watuhumiwa wote watatu ambao ni Joel joseph Nziku wa umri wa miaka 35 ambaye ni Dereva mkazi wa mtaa wa Magegere mjini Makambako ,Nasson Alfred Kaduma wa umri miaka 39 na Alphonce Edward Danda miaka 51 ambao wote ni wakulima na wakazi wa kijiji cha Ikando mnamo tarehe 20 mwezi wa kwanza waliwaua watoto watatu ambao ni Godliver Nziku,Gasper Nziku,na Glad nziku tukio ambalo walilifanya katika kijiji cha Ikando wilayani njombe . Hakimu mkazi wa mkoa wa njombe Magdalena Mtandu amesema kuwa kutokana na kosa hilo watuhumiwa hawapaswi kujibu chochote na kwamba watafikishwa mahakama kuu kujibu tuhuma zinazo wakabili upelelezi ukikamilika na kesi itatajwa tena hapo February 25 mwaka huu watuhumiwa wamerudishwa lumande kwa kuwa kesi hiyo haina dhamana. Nje ya mahaka mkuu wa oparesheni maalumu taifa Liberatus Sabas akizungumza vyombo vya habari amesema watuhumiwa wamauaji Wanaofikia 27 wataendelea kufikishwa mahakamani upelelezi ukikamilika na kwamba wakazi mkoa wa njombe waendelee kuishi kwa amani na ulinzi umeimaika.

Вы попали на страничку онлайн видео по фразе WATUHUMIWA MAUAJI WATOTO WA TATU KIJIJI CHA IKANDO WAFIKISHWA MAHAKAMANI. Если онлайн видео WATUHUMIWA MAUAJI WATOTO WA TATU KIJIJI CHA IKANDO WAFIKISHWA MAHAKAMANI Вам понравилось и Вы остались довольны результатом или наоборот, можете продолжить дискуссию комментарием ниже...

Мир в онлайне